Kwanza: Katiba
mpya itaje nchi zilizoungana: Tanganyika
na Zanzibar.
Isiwe kama ilivyo sasa. Isomeke: Tanzania
ni Jamhuri ya Muungano wa nchi mbili Tanganyika
na Zanzibar.
Pili: Serikali
iongozwe na Waziri Mkuu na Rais awe ni wa Heshima tu. Hii ni kuepusha mtu mmoja
kumiliki madaraka yote ya nchi ni pia kuongeza uwajibikaji.
Tatu: Kuwe na
mfumo wa majimbo ili kila mkoa ujiendeleze wenyewe isiwe kama
sasa bajeti ya ujenzi inajengwa Kigamboni tu; watu wa Kigoma wanafaidika nini?
Nne: Kuwe na
kikomo cha ubunge isiwe zaidi ya vipindiviwili au vitatu. Hii itamaanisha
wabunge watilie mkazo kuleta maendeleo na sio kujibakisha madarakani.
Tano: Wagombea
binafsi waruhusiwe wananci wasiwe watumwa wa vyama. Vyama vingine hata ni milki
ya watu wachache. Hii itaondosha uwezekano wa watu waxhaxhe kumiliki siasa za
nchi au kulazimiki kuabudu watu wengine ili wapate nafasi ya kugombea. Tanzania zio mali ya watu wachache.
Sita: Wananchi
wawe na uwezo wa kumuondoa mbunge madarakani endapo hawana imani nae tena.
Saba:
Katiba ipige marufuku mtumishi wa serikali asiekuwa raisi kutumia gari la umma
nje ya wakati wa kazi. Kuna baadhi ya wizara hutenga fedha za kuendeshea magari
nyingi zaidi ya fedha za kutoa huduma kwa umma.
Nane: Kiongozi
anaekumbwa na kashfa asimamishwe kazi kupisha uchunguzi. Aidha polisi wawe na
wajibu wa kuwachunguza watu wote wanaotuhumiwa bila ya kusubiri idhini ya
raisi. Kamanda atakeshindwa kuchunguza tuhuma zilizoenea mtaani ashitakiwe.
Tisa:
Mawaziri wasiwe wabunge ili kutoa mwanya wa kuteuwa watu wenye sifa zaidi. Pia
kuwapa wabunge uweo wa kuhoji bila ya tama ya uwaziri.
Kumi: Katiba
ipitishe makundi yote yaliyo nyma kimaendeleo yawekewe mikakati maalum ya
kuyaendeleza.
Kumi na moja:
Katika miiko ya uongozi kiongozi asiwe mbaguzi wala mchafu wa maadili. Mtu
anaetembea na watoto wa shule apoteze sifa ya kuwa kiongozi.
Kumi na mbili:
Kuhusu Muungano, muungano lazima uonyeshe nia njema. Hivi sasa mambo yote ya
kiuchumi yameingizwa ndani ya muungano na kuifanya Zanzibar
kama nchi iliyowekewa vikwazo; sasa mambo yote
ya muungano yapitiwe na baraza la wawakilishi.
Kuonesha kwamba hakuna nia njema, mafuta na gesi ni mambo ya
muungano, mbona almasi na dhahamu na makaa ya mawe sio ya muungano. Na hata
hiyo gesi mbona Zanzibar
haipewi fungu lake? Ikiwa dhahabu na almasi haviwezi kuwa vya muungano basin a
mafuta yatolewe.
Kwa nini kuwe na kodi mara mbili kwa nchi moja na mkusanyaji
mmoja. TRA hukuzanya kodi bandarini Zanzibar
halafu bidhaa hiyo hiyo watadai kodi bandarini Dar es Salaam. Hali hii ilipelekea kiwanda
cha sigara kuhamishswa kutoka Zanzibar kwa
sababu ilizuiliwa kupata soko Tanzania
bara.
Kwa vile hakuna nia njema. sasa muungano uwe wa mamlaka
tatu. Serikali ya Zanzibar, Serikali ya Tanganyika
na mamlaka ya muungao ambayo si lazima iwe na marais. iwe ni mkamishna tu
watakaoongozwa ama na Rais wa Zanzibar
au wa Tanzania Bara kwa mpishano.
Aidha kura ya maoni ipigwe iwapo wazanzibari au watanganyika
wanataka kuendelea na muungano. Muungano ni mtukufu lakini watu ni watukufu
zaidi wasilazimishwe kuungana kama wamechoka.
Aidha kwa kuwa watu ni watukufu zaidi ya Muungano waruhusiwe
kujadili Muunga wakati wowote bila ya vikwazo.
Kumi na tatu:
Tukiendelea na mfumo uliopo basi Rais iwe kwa zamu. Mara Zanzibar na mara nyengine atoke bara. Zanziba
tusiwe wadandiaji tu.
Kumi na nne:
Uongozi wa vyombo vya Muungano kama vile
Baraza la Mitihani, Jeshi la Wananchi na jeshi la Polisi uwe kwa uwiano wa sawa
kwa sawa.
Kumi na tano:
Bunge la Jamhuri lisijadili mambo ya bara. Wakati wa kujadili mambo ya Tanzania bara wawe wabara peke yao. Yaani watanganyika wawe na Bunge lao na Zanzibar lao. Halafu kuwe
na Bunge la Muungano
.