Saturday, July 21, 2012

MAONI YANGU KWA KATIBA MPYA


Kwanza: Katiba mpya itaje nchi zilizoungana: Tanganyika na Zanzibar. Isiwe kama ilivyo sasa. Isomeke: Tanzania ni Jamhuri ya Muungano wa nchi mbili Tanganyika na Zanzibar.
Pili: Serikali iongozwe na Waziri Mkuu na Rais awe ni wa Heshima tu. Hii ni kuepusha mtu mmoja kumiliki madaraka yote ya nchi ni pia kuongeza uwajibikaji.
Tatu: Kuwe na mfumo wa majimbo ili kila mkoa ujiendeleze wenyewe isiwe kama sasa bajeti ya ujenzi inajengwa Kigamboni tu; watu wa Kigoma wanafaidika nini?
Nne: Kuwe na kikomo cha ubunge isiwe zaidi ya vipindiviwili au vitatu. Hii itamaanisha wabunge watilie mkazo kuleta maendeleo na sio kujibakisha madarakani.
Tano: Wagombea binafsi waruhusiwe wananci wasiwe watumwa wa vyama. Vyama vingine hata ni milki ya watu wachache. Hii itaondosha uwezekano wa watu waxhaxhe kumiliki siasa za nchi au kulazimiki kuabudu watu wengine ili wapate nafasi ya kugombea. Tanzania zio mali ya watu wachache.
Sita: Wananchi wawe na uwezo wa kumuondoa mbunge madarakani endapo hawana imani nae tena.
Saba: Katiba ipige marufuku mtumishi wa serikali asiekuwa raisi kutumia gari la umma nje ya wakati wa kazi. Kuna baadhi ya wizara hutenga fedha za kuendeshea magari nyingi zaidi ya fedha za kutoa huduma kwa umma.
Nane: Kiongozi anaekumbwa na kashfa asimamishwe kazi kupisha uchunguzi. Aidha polisi wawe na wajibu wa kuwachunguza watu wote wanaotuhumiwa bila ya kusubiri idhini ya raisi. Kamanda atakeshindwa kuchunguza tuhuma zilizoenea mtaani ashitakiwe.
Tisa: Mawaziri wasiwe wabunge ili kutoa mwanya wa kuteuwa watu wenye sifa zaidi. Pia kuwapa wabunge uweo wa kuhoji bila ya tama ya uwaziri.
Kumi: Katiba ipitishe makundi yote yaliyo nyma kimaendeleo yawekewe mikakati maalum ya kuyaendeleza.
Kumi na moja: Katika miiko ya uongozi kiongozi asiwe mbaguzi wala mchafu wa maadili. Mtu anaetembea na watoto wa shule apoteze sifa ya kuwa kiongozi.
Kumi na mbili: Kuhusu Muungano, muungano lazima uonyeshe nia njema. Hivi sasa mambo yote ya kiuchumi yameingizwa ndani ya muungano na kuifanya Zanzibar kama nchi iliyowekewa vikwazo; sasa mambo yote ya muungano yapitiwe na baraza la wawakilishi.
Kuonesha kwamba hakuna nia njema, mafuta na gesi ni mambo ya muungano, mbona almasi na dhahamu na makaa ya mawe sio ya muungano. Na hata hiyo gesi mbona Zanzibar haipewi fungu lake? Ikiwa dhahabu na almasi haviwezi kuwa vya muungano basin a mafuta yatolewe.
Kwa nini kuwe na kodi mara mbili kwa nchi moja na mkusanyaji mmoja. TRA hukuzanya kodi bandarini Zanzibar halafu bidhaa hiyo hiyo watadai kodi bandarini Dar es Salaam. Hali hii ilipelekea kiwanda cha sigara kuhamishswa kutoka Zanzibar kwa sababu ilizuiliwa kupata soko Tanzania bara.
Kwa vile hakuna nia njema. sasa muungano uwe wa mamlaka tatu. Serikali ya Zanzibar, Serikali ya Tanganyika na mamlaka ya muungao ambayo si lazima iwe na marais. iwe ni mkamishna tu watakaoongozwa ama na Rais wa Zanzibar au wa Tanzania Bara kwa mpishano.
Aidha kura ya maoni ipigwe iwapo wazanzibari au watanganyika wanataka kuendelea na muungano. Muungano ni mtukufu lakini watu ni watukufu zaidi wasilazimishwe kuungana kama wamechoka.
Aidha kwa kuwa watu ni watukufu zaidi ya Muungano waruhusiwe kujadili Muunga wakati wowote bila ya vikwazo.
Kumi na tatu: Tukiendelea na mfumo uliopo basi Rais iwe kwa zamu. Mara Zanzibar na mara nyengine atoke bara. Zanziba tusiwe wadandiaji tu.
Kumi na nne: Uongozi wa vyombo vya Muungano kama vile Baraza la Mitihani, Jeshi la Wananchi na jeshi la Polisi uwe kwa uwiano wa sawa kwa sawa.
Kumi na tano: Bunge la Jamhuri lisijadili mambo ya bara. Wakati wa kujadili mambo ya Tanzania bara wawe wabara peke yao. Yaani watanganyika wawe na Bunge lao na Zanzibar lao. Halafu kuwe na Bunge la Muungano
.

No comments:

Post a Comment